Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Thursday 15 May 2014

YANAKUSHINDA KWASABABU MTAZAMO WAKO WA NDOA NI MBOVU



Nani alikwambia kuwa ndoa ni “show off”, kwani uliwaza nini kabla haujaoa au kuolewa naye? Nini kilochokufanya ufanye maamuzi magumu ya kumkubali kama mwenza maishani wakati bado moyoni ulikuwa unaona giza? Kama ulishawishiwa na wazazi au marafiki, wako wapi sasa wakati huu ambao wewe umesheheni huzuni? Au ni kwamba ulikuwa na matarajio makubwa kuliko uhalisia kwa huyo mwenzako? Angalia sasa ndoto zako zinafubaa!! Ukweli mnaujua nyie wenyewe kwamba sasa hivi mko ili kuonekana tu kama wenye ndoa vile kumbe hamna kinachoendelea, “no intimacy, no chemistry, everything is dead between you” tena mnatamani hata muanze kushuhulikia talaka, au kila mmoja aende kivyake lakini mnaogopa watu watawaonaje, status ya ndoa tu ndiyo inawaweka pamoja sasa hivi, mioyo na akili zenu zimejaa majuto. Kwa kujaribu kujiliwaza yamkini umeamua kujipooza kwa mchepuko lakini bado hata huo mchepuko haukupi furaha unayoitamani, ukiwaangalia watoto au mtoto wako unawaza labda niendelee kukaa kwenye hii ndoa kwa sababu yao. Au yamkini ndio mmeshafanikiwa kuachana kabi, umri mdogo lakini umeshabadili “status” unaitwa mtaliki au mtalikiwa “divorced”. Najua inauma na ni ngumu sana kwenu, na kweli ninastahili kukwambia pole sana lakini nivema nikuulize swali moja kabla ya kukupa hiyo pole “Je unajua ulikokosea????” kama hujawahi kujiuliza swali hili basi utakuwa mtaalamu “expert” wa kuachwa na kuacha kwasababu kwa kawaida tukijikwaa hata kama tutoke damu kiasi gani, mtazamo wetu hatuuweki kwenye kidole kilichoumia bali kwenye jiwe lililotukwaza, ili kesho au keshokutwa tusijikwae tena. Kosa angalau liwe mara moja, yanapozidi unakuwa umbulula wa kawaida tu. Tafakari, chukua hatua – Chris Mauki

No comments:

Post a Comment

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive