Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Tuesday 27 May 2014

HAIJALISHI UNAPITIA MAUMIVU GANI YA PENZI, BADO LIPO TUMAINI



Haijalishi sana jinsi ndoa yenu ilivyokuwa siku mlipokuwa mnaoana, kinachojalisha zaidi ni katika jinsi mnavyoishi wawili ndani ya ndoa hiyo, kiukweli inawezekana kabisa ndoa yenu ilikuwa ni story ya mjini, ukumbi wa garama sana, mapambo bei hielezeki, mc the best of the town, gari yenu peke yake ilikuwa bajeti ya harusi ya mtu mwingine na hanymoon mkaenda ulaya, Dubai au Capetown au kokote unakohisi ni kwa gharama na pa kuvutia sana, lakini ukiyaangalia maisha mnayoishi wote baada ya matumizi haya yote ya fedha za wasamaria wema walioamua kuzipotezea kwenu, unaona furaha ile iliishia ukumbini au ilidumu kwa wikichache sana baada ya fungate, machungu na maumivu ya moyo unayoyapitia yanakufanya uone aibu hata kuziangalia picha zenu na mikanda yenu ya harusi. Sio bestman, matron wala wazazi wenu wanaojua chungu mnayoipitia, ukiuangalia moyo na nafsi yako unatamani kuilaani siku ile uliyomkumbatia na kucheza naye muziki wa taratibu ukumbini huku watu wakidhani “wapendanao wawili wamekutana”. Ngoja nikutie moyo, najua kweli kuna sehemu ulikosea au mlikosea, najua majuto karibu yafunike matarajio yako, lakini lipo tumaini, maadam bado mnapumua, basi mnaweza kuyarekebisha na mkaiona tena ile furaha ya mwanzo kama kweli wote mnadhamiria kuitafuta furaha hiyo. “It takes two to tango” Pasipo nia ya dhati ya wote wawili, furaha hii bado itakuwa ni kitendawili. Nyanyuka, futa machozi, chukua hatua, tumaini bado lipo – Chris Mauki.

No comments:

Post a Comment

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive