Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Thursday 3 July 2014

JE UNAUJUA UNDANI WA KISAIKOLOJIA KUHUSU “ORAL SEX”???



Watafiti wa chuo kikuu cha McGill nchini Marekani wamegundua kwamba wapenzi wengi hugombana na kutofautiana kuhusu suala la kunyonyana “oral sex” hii ni kutokana na mmoja kutamani zaidi kufanyiwa wakati mwingine hapendi au hufanyi kama mwenzake anavyotaka. Utafitii huu unaonyesha kwamba “oral sex” husisimua na kuamsha kuliko tendo la ndoa la kawaida “intercourse” na wanaume huhemka zaidi katika “oral sex” kuliko wanawake. Sababu kubwa ya hisia hii ya pekee kwa wanaume ni kwamba “lips”, ulimi na vidole vya mwanamke huamsha na kupanua “urethral” ya mwanaume, na hii humfanya mwanaume ajisikie kuhemka sana tofauti na uume unapokuwa ndani ya uke. Ni kweli kwamba jinsi mwanaume anapoongeza kuhemka sehemu yake ya juu kabisa ya uume “the tip area” hupunguza uwezo wa kuhisi, uume huwa na kitu kama ganzi, wataalam wanasema hii ni njia asilia aliyoifanya Mungu ya kumsaidia mwanaume asiumie hususani wakati uume ukiwa ndani ya uke “during intercourse”. Kwahiyo watafiti hawa wanasema kama mara nyingine mwanaume hafiki kileleni kwa tendo la ndoa la kawaida labda anaweza kufikia kupitia “oral sex”. Nasisitiza kwamba utafiti huu haukuhusisha vitu kama imani au utamaduni wa watu – Chris Mauki.

Thursday 26 June 2014

AINA TANO ZA KUACHANA KATIKA MAPENZI (5 ways to breakup)




1. Kuchemka hadi kumwagika "The Boil Over"

Katika hali hii unaanza kuziona dalili za kuachana kwenu kwa mbali. Labda mwenzako amekuwa akifanya au kusema vitu fulani kwa muda mrefu na vimekuwa havikufurahishi, kila unapotaka kumpasukia kunakitu kinakwambia “subiri, mpe nafasi nyingine”, ndani yako unajiona kabisa kuwa wakati umewadia sasa wa kumpasha habari yake kwa mara ya kwanza na ya mwisho, na pia ndani yako unakuwa na utayari wa kubeba majukumu kwa chochote utakachomwambia. Gafla sikumoja kinatokea kitu kidogo tu, labda ni neno lililosemwa au kitu kilichofanywa na wewe au mpenzi wako, mnagombana na kutofautiana sana na kutokana na machungu na maumivu ya muda mrefu moyoni mmoja anaamua kuutumia upenyo huo kulitamka neno “it’s over” (naomba tuachane) na huo unakuwa mwisho wa penzi lenu. 

2. Kuachana kimlipuko

Yako baadhi ya mahusiano ambayo huwa yana vipindi vya amani kwa kitambo kidogo na milipuko ya magomvi kwa kipindi kingine. Milipuko hii simaanishi kule kutoelewana kwa kawaida bali mahusiano yanakumbwa na milipuko ya kutoelewana kwa kitu fulani kizito, au ugomvi unakuwa mzito na wenye kuyumbisha pande zote mbili. Kwa mfano baada ya kitambo cha amani na mapenzi kunagundulika kuwepo kwa mahusiano ya pembeni kwa mmoja wa wapenzi (cheating) na hili linazua mlipuko wa ugomvi ambao gafla unalizima penzi na ule ukaribu wenu unafifia ghafla na kutokomea jumla. Yamkini ni mlipuko mmoja tu umetokea lakini mpenzi mmoja aliyeumizwa hatamani hata kumwona mwenzake kwa macho, wapendanao hawa wanajeuka maadui ghafla (one blow away).


3. "Leo nje kesho ndani, kesho baridi keshokutwa moto”
Hii ni staili ya kuachana ambayo wengi wetu huitumia mara kwa mara na maranyingine pasipo muhusika mmoja katika penzi kufahamu kwamba safari ya kuachana ndo inawadia. Katika mahusiano ya watu wa namna hii kunakuwa na mazingira yanayo wafanya leo wanakorofishana kesho wanapatana, kesho wanakuwa pamoja keshokutwa unaskia hawapo tena pamoja, mara unasikia wamerudiana, tena wanakuja kufarakana na tabia hii inakuwa ndo maisha yao ya kilasiku na mfumo wa mahusiano yao. Tabia hii huendelea kudumu hadi inafika nyakati mmoja akitoka basi anatoka jumla, kila mwenzake akiwaza kwamba yamkini atarudi kama mazoea yao yalivyo lakini haiwi hivyo tena na penzi lao linakatikia hapo. 



4. "Mkate ulioungua”
Mara nyingi tunapopika mkate huuweka kwenye joto kali ili uive na mara kwa mara muokaji huuangalia kama umeiva kwa kuutumbukizia kitu kikali kama vile uma ili kuangalia hali yake ya ndani ilivyo na kufahamu maendeleo ya uivaji wake. Mkate uliosahaulika kuangaliwa mara kwa mara huungua na muokaji anapokuja kuutoboa ndipo anapofahamu kuwa mambo yameshaharibika kuanzia ndani na mkate haufai kuliwa tena.
Katika mahusiano yetu  hususani kwa baadhi ya wale walioweza kukaa muda mrefu au hata waliooana, bahati mbaya kwasababu ya masumbufu ya maisha ya kilasiku na mapenzi ya kimazoea wakasahau kuchochea na kuziamsha hamasa za penzi lao kila mara, penzi hilo taratibu hushuka na kupoa ladha na taratibu pasipo wapendanao hawa kugundua kilakitu kinakuwa chabaridi, kilichoganda, kisicho na ladha na kilammoja akitamani penzi la ladha ya tofauti kutoka kwa mtu wa tofauti. Hii inapelekea wawili hawa kuchagua kuachana.

5. "Ghafla moto ghafla baridi”
Kama umewahi kutumia mashine ya kupashia joto chakula “microwave” utaelewa kitu ninachojaribu kuzungumza hapa, tabia ya mashine hii ni kupasha joto chakula kwa haraka sana na marakikitoka huweza kupoa kwa haraka zaidi pia. Yako mapenzi ambayo yameanzishwa gafla sana (kwa muda mfupi sana) na yaka paa juu sana, kila mmoja akimhisi mwenzake kiukaribu sana, na hisia za wawili hawa zinakuwa za moto kama zilizo wekwa kwenye ‘microwave’ lakini ghafla mmoja kati ya wapendanao hawa anazimika na kutoendeleza tena moto uliokuwepo. Kwa mfano mlianza gafla kuhusiana na mapenzi yakawa moto kuliko mlivyofikiri, kilasiku mkowote na lazima muonane au muwasilianer kwa simu, ghafla mwenzako hapokei simu, na wala akiiona simu yako hawajibiki kukupigia au kukwambia nini kinaendelea, na tabia hiyo inaendelea hivyohivyo hadi unakata tama na unaamua kukubali yaishe. Mapenzi haya yaliwaka na kuzima kwa mtindo wa microwave.

Wakati unahisi penzi lenu linafikia mwisho nivema mkafikiri njia bora za kuachana na maranyingine ikibidi kuliongea hili kwa pamoja. Baadhi ya njia nyingine zinawezakuwa na madhara makubwa nay a muda mrefu kwa wahusika au muhusika mmoja na nyingine madhara yake ni madogo na yasiyo ya muda mrefu. Wakati wote tunashauri kuachana isiwe ndiyo njia mbadala ya kwanza (first altenative) bali jitihada za kusuluhisha na kubadilika tabia ziangaliwe kwanza na kupewa kipaumbele na kila anayehusika katika penzi. Kumbuka kuwa katika jitihada za kubadili tabia ni zoezi linalotakiwa kusaidiana baina ya wawili wapendanao na sio kazi ya mtu mmoja.  
Nakutakia kufanikiwa zaidi katika mahusiano yako na sio kukimbilia kuachana.

Na: Chris Mauki. Social, Relationships and Counselling Psychologist.

Friday 20 June 2014

HARUSI YA VICTOR GEORGE MKUCHIKA NA MKEWE ELIZABETH. DIAMOND JUBILEE VIP HALL 14.6.2014

 Director of the event Chris Mauki akiratibisha shuhuli nzima
 Kwaweli Diamond jubilee ilipendeza
 High table kabla ya Victor na Elizabeth kuingia
 Victor na Elizabeth wakiingia ukumbini
 Bride maids nao wakiingia
 Mh. George Mkuchika na mke wake wakipokea keki toka kwa Elizabeth
 Bwana Jenerali Ulimwengu naye alikuwepo
 Waziri mkuu mstahafu Jaji Joseph Warioba na mkewe walikuwepo pia
Mandhari safi ya Diamond jubilee VIP Hall inavyoonekana sasa

Monday 16 June 2014

JE UKUBWA AU UDOGO WA MAUMBILE YA KIUME UNAHUSU?



Mtaalam  ubongo Boizendine anasema kuwa uume “penis” wakati wowote huchukua nafasi kubwa sana katika kuwazwa au kufikiriwa  akilini mwa wanaume na wanawake kuliko vitu vingine vingi, lakini inapofika katika suala la tendo la ndoa, ukubwa au udogo wa uume “size of penis” sio suala la muhimu sana tofauti na jinsi wanaume wengi wanavyolichukulia na kulihofia. Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume hutumia nguvu nyingi zaidi kuwaza na kuhofu kuhusiana na ukubwa au udogo wa maumbile yao “size of the penis” kuliko wanavyo waza kuhusu kufanya mapenzi. Hata hivyo zaidi ya asilimia 85 ya wanaume wameonyesha kutamani kuwa na uume mkubwa, wakati wapenzi wengi wa wanaume hawa wameonyesha kuridhika na hali ya uume wa wapenzi wao. Wanawake hawa wanasema kuwa wao huhemshwa au kuwa “turned on” kimapenzi na viungo vingine vya mwanaume kama vile macho yao, tabasamu, misuli na namna midomo yao ilivyo na wala sio suala la uume. Hii itawasaidia badhi ya wanaume kubadili mtazamo wao kwamba “size” ya uume ndio kitu cha muhimu zaidi. Watafiti wanasema kipimo cha wastani cha uume wa mwanaume ni kati ya inchi 5.5 hadi 6.2, kwahiyo futilia mbali hofu zako usije kushindwa kufanya kazi nyingine za msingi – Chris Mauki.

Saturday 14 June 2014

KITABU CHA JITAMBUE KISAIKOLOJIA SASA NDANI YA MLIMANI CITY

Wale wapenzi na wasomaji wa kazi za Chris Mauki sasa mnaweza kukipata kitabu hiki cha JITAMBUE KISAIKOLOJIA: HATUA KWA HATUA KUELEKEA MAFANIKIO YA KWELI pale Mlimani City kwenye duka la vitabu la MAK SOLUTIONS kwa bei ni ile ile ya sh 10000?= tu. Kitabu hiki kitayabadilisha maisha na mtazamo wako.

Thursday 12 June 2014

TOFAUTI YA MUDA WA FAMILIA NA MUDA WA MPENZI WAKO



Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na muda na mpenzi wako "quality time with your love" na kuwa na muda na familia "quality time with your family". Wanaume wengi huwa wanadhani wakishakuwa na muda na familia zao ndo wamemaliza, wanafikiri kwa kule kukaa hotelini na familia nzima mke naye tayari kashapata muda wake na kiu yake imekata, kumbe kwa mwanamke ule ulikuwa muda wa wewe na yeye na watoto kwa pamoja, bado muda wa wewe kuwa na yeye peke yenu. Yako mambo ambayo kama wanandoa hamuwezi kuyazungumza mkiwa na watoto bali mkiwa peke yenu tu, na mara nyingine hata kama hamna la kuzungumza bado mnahitaji muda wa kuwa peke yenu. Kamwe muda wako mume na familia yako hauwezi kumridhisha mkeo kama ambavyo mngepata muda na yeye peke yake. Wives needs quality time with their husbands independently from the children, husbands’ dont hide in the shadow of the kids – Chris Mauki

Wednesday 11 June 2014

UTOFAUTI WA KIASILI ULIOPO KATIKA KIU NA UWEZO WA KUFANYA MAPENZI BAINA YA WANAWAKE NA WANAUME



Watafiti waliowahoji wanaume katika jamii na familia tofauti wameonyesha kwamba wanaume kwa kawaida huweza kukutana kimapenzi na wanawake 14 na kuendelea katika kipindi cha maisha yao, wakati wanawake wameonyesha kutamani au kuweza kukutana na mwanaume moja au wawili katika kipindi cha maisha yao. Kuzidi kuongezeka kwa idadi kwa wanaume inasemekana ni kutokana na kiu yao ya kuweza kufurahia ngono ya sikumoja au ya usiku mmoja “one-night stand” tofauti na wanawake ambao wao hutamani zaidi kule kumaanisha katika penzi hilo. Utafiti huu umeangalia zaidi kiu ya kufanya mapenzi ya kiasili na sio kwasababu ya msukumo wa uhitaji au umasikini ambapo wanawake wengi hujikuta wanafanya mapenzi zaidi (hata pale ambapo hawakutamani kufanya au hata wasipolifurahia tendo hilo) ili tu kupata mahitaji yao ya kila siku – Chris Mauki.

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive