Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Thursday 26 June 2014

AINA TANO ZA KUACHANA KATIKA MAPENZI (5 ways to breakup)




1. Kuchemka hadi kumwagika "The Boil Over"

Katika hali hii unaanza kuziona dalili za kuachana kwenu kwa mbali. Labda mwenzako amekuwa akifanya au kusema vitu fulani kwa muda mrefu na vimekuwa havikufurahishi, kila unapotaka kumpasukia kunakitu kinakwambia “subiri, mpe nafasi nyingine”, ndani yako unajiona kabisa kuwa wakati umewadia sasa wa kumpasha habari yake kwa mara ya kwanza na ya mwisho, na pia ndani yako unakuwa na utayari wa kubeba majukumu kwa chochote utakachomwambia. Gafla sikumoja kinatokea kitu kidogo tu, labda ni neno lililosemwa au kitu kilichofanywa na wewe au mpenzi wako, mnagombana na kutofautiana sana na kutokana na machungu na maumivu ya muda mrefu moyoni mmoja anaamua kuutumia upenyo huo kulitamka neno “it’s over” (naomba tuachane) na huo unakuwa mwisho wa penzi lenu. 

2. Kuachana kimlipuko

Yako baadhi ya mahusiano ambayo huwa yana vipindi vya amani kwa kitambo kidogo na milipuko ya magomvi kwa kipindi kingine. Milipuko hii simaanishi kule kutoelewana kwa kawaida bali mahusiano yanakumbwa na milipuko ya kutoelewana kwa kitu fulani kizito, au ugomvi unakuwa mzito na wenye kuyumbisha pande zote mbili. Kwa mfano baada ya kitambo cha amani na mapenzi kunagundulika kuwepo kwa mahusiano ya pembeni kwa mmoja wa wapenzi (cheating) na hili linazua mlipuko wa ugomvi ambao gafla unalizima penzi na ule ukaribu wenu unafifia ghafla na kutokomea jumla. Yamkini ni mlipuko mmoja tu umetokea lakini mpenzi mmoja aliyeumizwa hatamani hata kumwona mwenzake kwa macho, wapendanao hawa wanajeuka maadui ghafla (one blow away).


3. "Leo nje kesho ndani, kesho baridi keshokutwa moto”
Hii ni staili ya kuachana ambayo wengi wetu huitumia mara kwa mara na maranyingine pasipo muhusika mmoja katika penzi kufahamu kwamba safari ya kuachana ndo inawadia. Katika mahusiano ya watu wa namna hii kunakuwa na mazingira yanayo wafanya leo wanakorofishana kesho wanapatana, kesho wanakuwa pamoja keshokutwa unaskia hawapo tena pamoja, mara unasikia wamerudiana, tena wanakuja kufarakana na tabia hii inakuwa ndo maisha yao ya kilasiku na mfumo wa mahusiano yao. Tabia hii huendelea kudumu hadi inafika nyakati mmoja akitoka basi anatoka jumla, kila mwenzake akiwaza kwamba yamkini atarudi kama mazoea yao yalivyo lakini haiwi hivyo tena na penzi lao linakatikia hapo. 



4. "Mkate ulioungua”
Mara nyingi tunapopika mkate huuweka kwenye joto kali ili uive na mara kwa mara muokaji huuangalia kama umeiva kwa kuutumbukizia kitu kikali kama vile uma ili kuangalia hali yake ya ndani ilivyo na kufahamu maendeleo ya uivaji wake. Mkate uliosahaulika kuangaliwa mara kwa mara huungua na muokaji anapokuja kuutoboa ndipo anapofahamu kuwa mambo yameshaharibika kuanzia ndani na mkate haufai kuliwa tena.
Katika mahusiano yetu  hususani kwa baadhi ya wale walioweza kukaa muda mrefu au hata waliooana, bahati mbaya kwasababu ya masumbufu ya maisha ya kilasiku na mapenzi ya kimazoea wakasahau kuchochea na kuziamsha hamasa za penzi lao kila mara, penzi hilo taratibu hushuka na kupoa ladha na taratibu pasipo wapendanao hawa kugundua kilakitu kinakuwa chabaridi, kilichoganda, kisicho na ladha na kilammoja akitamani penzi la ladha ya tofauti kutoka kwa mtu wa tofauti. Hii inapelekea wawili hawa kuchagua kuachana.

5. "Ghafla moto ghafla baridi”
Kama umewahi kutumia mashine ya kupashia joto chakula “microwave” utaelewa kitu ninachojaribu kuzungumza hapa, tabia ya mashine hii ni kupasha joto chakula kwa haraka sana na marakikitoka huweza kupoa kwa haraka zaidi pia. Yako mapenzi ambayo yameanzishwa gafla sana (kwa muda mfupi sana) na yaka paa juu sana, kila mmoja akimhisi mwenzake kiukaribu sana, na hisia za wawili hawa zinakuwa za moto kama zilizo wekwa kwenye ‘microwave’ lakini ghafla mmoja kati ya wapendanao hawa anazimika na kutoendeleza tena moto uliokuwepo. Kwa mfano mlianza gafla kuhusiana na mapenzi yakawa moto kuliko mlivyofikiri, kilasiku mkowote na lazima muonane au muwasilianer kwa simu, ghafla mwenzako hapokei simu, na wala akiiona simu yako hawajibiki kukupigia au kukwambia nini kinaendelea, na tabia hiyo inaendelea hivyohivyo hadi unakata tama na unaamua kukubali yaishe. Mapenzi haya yaliwaka na kuzima kwa mtindo wa microwave.

Wakati unahisi penzi lenu linafikia mwisho nivema mkafikiri njia bora za kuachana na maranyingine ikibidi kuliongea hili kwa pamoja. Baadhi ya njia nyingine zinawezakuwa na madhara makubwa nay a muda mrefu kwa wahusika au muhusika mmoja na nyingine madhara yake ni madogo na yasiyo ya muda mrefu. Wakati wote tunashauri kuachana isiwe ndiyo njia mbadala ya kwanza (first altenative) bali jitihada za kusuluhisha na kubadilika tabia ziangaliwe kwanza na kupewa kipaumbele na kila anayehusika katika penzi. Kumbuka kuwa katika jitihada za kubadili tabia ni zoezi linalotakiwa kusaidiana baina ya wawili wapendanao na sio kazi ya mtu mmoja.  
Nakutakia kufanikiwa zaidi katika mahusiano yako na sio kukimbilia kuachana.

Na: Chris Mauki. Social, Relationships and Counselling Psychologist.

No comments:

Post a Comment

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive