Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Wednesday 28 May 2014

ANOTHER HOT TALK IN TOWN "THE COURAGE TO GROW" VCCT. 1 JUNE 2014

Hii sio ya kukosa, bureeeeeeeeee, ushalipiwaaaaa

TAKWIMU YA NCHI ZINAZOONGOZA KUTEMBELEA BLOG YETU


Shukrani kwa wote ambao wanatupa support Tambua kuwa Bila nyie tusingekuwa hapa 
Tunawapenda sana

God Bless you all

Tuesday 27 May 2014

HAIJALISHI UNAPITIA MAUMIVU GANI YA PENZI, BADO LIPO TUMAINI



Haijalishi sana jinsi ndoa yenu ilivyokuwa siku mlipokuwa mnaoana, kinachojalisha zaidi ni katika jinsi mnavyoishi wawili ndani ya ndoa hiyo, kiukweli inawezekana kabisa ndoa yenu ilikuwa ni story ya mjini, ukumbi wa garama sana, mapambo bei hielezeki, mc the best of the town, gari yenu peke yake ilikuwa bajeti ya harusi ya mtu mwingine na hanymoon mkaenda ulaya, Dubai au Capetown au kokote unakohisi ni kwa gharama na pa kuvutia sana, lakini ukiyaangalia maisha mnayoishi wote baada ya matumizi haya yote ya fedha za wasamaria wema walioamua kuzipotezea kwenu, unaona furaha ile iliishia ukumbini au ilidumu kwa wikichache sana baada ya fungate, machungu na maumivu ya moyo unayoyapitia yanakufanya uone aibu hata kuziangalia picha zenu na mikanda yenu ya harusi. Sio bestman, matron wala wazazi wenu wanaojua chungu mnayoipitia, ukiuangalia moyo na nafsi yako unatamani kuilaani siku ile uliyomkumbatia na kucheza naye muziki wa taratibu ukumbini huku watu wakidhani “wapendanao wawili wamekutana”. Ngoja nikutie moyo, najua kweli kuna sehemu ulikosea au mlikosea, najua majuto karibu yafunike matarajio yako, lakini lipo tumaini, maadam bado mnapumua, basi mnaweza kuyarekebisha na mkaiona tena ile furaha ya mwanzo kama kweli wote mnadhamiria kuitafuta furaha hiyo. “It takes two to tango” Pasipo nia ya dhati ya wote wawili, furaha hii bado itakuwa ni kitendawili. Nyanyuka, futa machozi, chukua hatua, tumaini bado lipo – Chris Mauki.

Monday 26 May 2014

JE UNAMAPENZI NA KAZI UNAYOIFANYA TOKEA MOYONI? AU UNAIFANYA KWASABABU UMELAZIMIKA KUWA KWENYE HIYO KAZI?



Kunatofauti kubwa sana kati ya kufanya kazi na kufanya kazi unayoipenda na uliyoitamani tokea mbali. Zaidi ya asilimia 85 ya watu hufanya kazi wasizozipenda au ambazo hawakuwahi kuzitarajia kuja kuzifanya na hii inawapa kukosa furaha na utoshelevu “satisfaction” katika kile wakifanyacho hata kama kinaonekana ni kizuri na chenye kuwalipa. Ogopa sana na epuka kabisa kuishia kwenye kazi au ajira ambayo huna mapenzi nayo tokea moyoni mwako, usije kuishia kukifanya kile unachokipenda na kukitamani ukishastaaafu hicho unachokifanya sasa, kwamaana muda wakukifanya kile ukipendacho utakuwa ni mdogo na mfupi sana wakati ulifanya usichokipenda kwa muda mrefu maishani mwako. Kati ya vitu viwili muhimu kuvifurahia maishani ni familia yako, na kazi unayoifanya. Jifunze kufanya chaguzi bora, kuweka malengo bora na kufanya maamuzi bora iwapo mapema – Chris Mauki.

FAHAMU UTOFAUTI WA MAUMIVU AYAPATAO MWANAUME NA MWANAMKE PALE WANAPOGUNDUA KUWA WANASALITIWA



Wivu na maumivu anayoyasikia mwanamke pale anapohisi au kugundua kuwa mpenzi wake wa kiume anatembea nje ya mahusiano yao uko katika kiwango cha hisia “emotional level” wakati maumivu anayoyapata mwanaume kwa kusikia au kugundua kuwa mpenzi wake wa kike anamtu mwingine uko katika kiwango cha himaya “territorial level”. Wakati mwanamke anaumia kwa wivu akijiuliza kwanini mwanaume wangu achukuliwe na mwanamke mwingine, huku akiwa na kiu ya kumjua huyo mwanamke anafananaje? Ananini? Anauwezo gani kimvuto na kimuonekano? Maswali haya moyoni mwake huongeza maumivu katika hisia za mwanamke huyu, kwa upande wa pili mwanaume haumii hihisia lakini huumia na kupata machungu zaidi ya mwanamke huku moyoni mwake akihisi kushindwa kuimiliki himaya yake vema hadi mwanaume mwingine kuweza kuivamia, hujihisi kama askari aliye na silaha dhaifu au aliyeshindwa kutumia silaha zake vema hadi askari wa kambi nyingine akapata urahisi wa kumvamia tena kwenye kitovu cha kambi yake. Katika hali hizi, mwanamke humtazama mwanaume wake kama mpenzi wakati mwanaume akimtazama mwanamke wake kama himaya. Ni ngumu sana mwanaume kustahimili maumivu ya jinsi hii, na ndio maana kwa wanaume wengine huwa rahisi hata kuwaza kujitoa uhai au kuutoa uhai wa huyo mwanaume mwingine aliyetembea na mpenzi wake, wapo pia wanaume ambao huishiwa nguvu za kufanya tendo la ndoa kwa muda fulani “temporary impotency” mara tu wanapogundua kusalitiwa, na nimeshuhudia mwanaume aliyeamua kuzikata sehemu zake zote za siri kwasababu ya kuona hazina tena umuhimu, ingawa hakuweza kuishi tena baadae. Maumivu na matendo haya hayafanyiki sana kwa jinsia ya kike, wao huishia zaidi kulia, kupiga kelele sana, kutukana, na juhudi za kumsaka huyo mwanamke mwingine zikifanikiwa basi wanaweza kupigana kidogo na kuwekeana uadui wa kawaida, ambao sikumoja unaweza ukaisha - Chris Mauki.

EXTRA-CURRICULA ACTIVITIES: NDANI YA UKUMBI WA URAFIKI SOCIAL HALL JUMAMOSI 24.5.2014




Friday 23 May 2014

UHUSIANO WA KULA NYAMA NA TENDO LA NDOA (MEAT FOR SEX PRINCIPLE)



Katika utafiti juu ya tabia za binadamu zinazohusiana na tendo la ndoa “sex” wataalam wa kibaiolojia wamegundua kwamba wanakwake wengi wamejikuta wanakubali kufanya mapenzi na wanaume ambao waliwaletea, waliwalisha au kuwanunulia nyama, wataalam hawa wameiita hii ni “meat for sex principle”. Katika utafiti mwingine unaofanana na huu unaonyesha kwamba wanaume walioonyesha utayari na uwezo wa kuhakikisha wanawake wao wanashiba (wanakula na kunywa watakavyo) wamekuwa wakipewa tendo la ndoa kiurahisi zaidi kuliko wanaume wengine walioonyesha udhaifu kwenye jambo hilo, kwahiyo kiasili kwa wewe mwanamke ukiona jamaa anakukaribisha nyama choma mara kwa mara ujue kabisa mnakoelekea – Chris Mauki

DODOMA KUWAKA MOTO JUMAPILI HII TAR 25-5-2014



Dodoma jumapili hii tar 25.5.2014. royal village hotel kuanzia saa 8:30 ,mchana. Nitakuwa nafundisha jinsi ya kujenga mahusiano yenye afya (Building a healthy relationship). Mwambie na mwenzako. Vitabu vya jitambue kisaikolojia vitapatikana pia. Chris Mauki na Haris Kapiga watazungumza. ni kwa sh 15000 tu.

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive