Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Tuesday 20 May 2014

TOFAUTI KATI YA WANAWAKE NA WANAUME KATIKA KUSUBIRI TENDO LA NDOA



Tafiti zinaonyesha kwamba mara mwanaume anapovutiwa na mwanamke kimapenzi gafla huamsha hamu yake ya kufanya mapenzi na kutamani kufanya tendo hilo haraka iwezekanavyo. Kwa mwanaume katika hali hii kusubiri siku chache au hata wiki moja ni mtihani mgumu sana, lakini upande wa pili, mwanamke huwa na kiu na uwezo mkubwa wa kusubiri mara tatu zaidi ya uwezo wa wanaume. Hii itakusaidia kujua ni kwasababu gani wanaume wengi mara wakikutana na mwanamke wakavutiwa naye, hulazimisha na kuweka kila mazingira kuhakikisha wanafanya mapenzi tena ikiwezekana siku hiyo hiyo, hata kama mazingira hayaruhusu, na mara nyingi akishafanikiwa kufanya jambo hilo gafla hubadilika, mtazamo wake, ahadi zake, na kumaanisha kwake huwa tofauti na maneno pamoja na matendo aliyoyaonyesha kabla hamjafanya mapenzi, na hapa ndipo wanawake wengi huumizwa sana moyo na hisia zao na kuwaita wanaume wasaliti na waumizaji. Labda kwa kujua hili itakusaidia wewe mwanamke ambaye labda ulifikiri kule kusisitiza na kulazimisha shauku yake ya kufanya mapenzi na wewe ukadhani ni upendo wake wa dhati, watch out usijekuwa tajiri wa machozi. Kumbuka “Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake” – Chris Mauki

1 comment:

  1. Aisee hii somo zuri. Natamani wengine wangelipata.

    ReplyDelete

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive