Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Monday 19 May 2014

JIHADHARI MAHUSIANO YAKO YANAPOONYESHA TAA NYEKUNDU




Kama unaona mawasiliano baina ya wewe na mpenzi wako yanaelemea zaidi kwenye kuzungumzia masuala kama vile, watoto, kazi, biashara, pesa, ndugu, mashamba, ujenzi, mifugo, elimu za watoto, afya ya watoto, gesi imeisha, na masuala mengine ya nyumbani kama vile hiki kiko wapi na kile kikowapi, au labda mwenzi wako akiwa hayupo nyumbani akikupigia simu au kukutumia ujumbe anauliza tu watoto wanaendeleaje? Nyie mko salama? Hana kiu nyingine yakutaka kujua zaidi kuhusu wewe kama mpenzi wake na hisia zako, na wala wewe hauna kiu ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu yeye anaendeleaje, hisia zake huko aliko, na kujua kama anakukumbuka au la, unaishia tu kumjibu maswali yake, “ndiyo hawajambo”!! “kila kitu kiko sawa kwaheri”!!. Ukiona mawasiliano au maongezi ya namna hii yanazidi mawasiliano baina yenu kuhusu nyie wenyewe binafsi, mahusiano yenu na penzi lenu, na pia kama muda wenu wa kuketi kuzungumza hayo mambo niliyoyataja awali unazidi ule muda wenu wa kuzungumza mambo yenu binafsi, basi kuna uwezekano mkubwa mahusiano yenu yako wodini, na inawapasa muwe macho sana na hali hii kwasababu hapo kuna mawili, aidha mahusiano yenu yakitoka wodini yaende kwenye chumba cha wagonjwa mahututi “ICU” au yakaenda mochwari “mortuary” kabisa. Haya sasa kazi kwenu kumuokoa mgonjwa wenu – Chris Mauki

1 comment:

  1. NDOA NGUMU KAKANGU!

    WAZO LA LEO: WANAUME WAJIFUNZE KUPENDA WAKE ZAO KAMA MAANDIKO YALIVYO WAELEKEZA MAANA HISIA ZA MWANAMKE HAZIPO KITANDANI NI SERIES TOFAUTI NA MWANAUME ANAWEZA KUFANYA MAPENZI NA KICHAA AU CHANGU DOA HANA HISIA NAE LKN KWA MWANAMKE MPAKA AFANYE MAPENZI NA MWANAUME AMEPATA HISIA JUU YAKE NI SERIES.

    WATCH OUT WANAUME! COZ WANAWAKE NA SISI YAKITUKABA TUNASHINDWA KURIDHIKA NA KURIDHISHA MATOKEO YAKE MAHUTUTI/MOCHWARI NA NDOA ZINATUSHINDA.

    ReplyDelete

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive