Inawezekana sana ukaishi na watoto au mtoto wako nyumbani lakini
akahisi kama vile haupo. Labda kwa lugha nyingine naweza kusema unaweza
kuwepo nyumbani kimwili “physically” lakini usiwepo kihisia na kijamii
“absent socially and emotionally” na hapa ndipo wazazi na walezi wengi
tulipo pasipo kujua na huku tukidhani kuwa mambo yote baina yetu na
watoto wetu yako sawa, ukweli ni kwamba hali sio shwari hata kidogo na
kwa bahati mbaya mbegu hii mbovu inayopandwa wakati huu inaota na kumea
na kuleta uharibifu wa kudumu katika maisha yote ya mwanao au wanao.
Nakushauri ujifunze kubadilika.
Hapa nina vitu vichache ambavyo ni
mifano tu ya jinsi au namna ya kukuza na kuendeleza ukaribu au uhusiano
baina ya wewe mzazi na mtoto wako. Nina watoto wawili wakike lakini
nyumbani kwangu huwa kuna watoto zaidi ya wawili mara nyingi. Hii ni
kwasababu watoto hawa toka nyumba za jirani wamejenga uhusiano mzuri wa
mzazi na mtoto “parent-child relationship” na mimi kuliko walivyo jenga
na wazazi wao, kwahiyo kwao kukaa nyumbani kwangu, wakila, kunywa na
kufurahia urafiki na hali ya wao kuwa katika “familia” kunawafanya
washinde kwengine mchana na wakalale kwingine usiku. Unaweza kutengeza
mazingira ya wanao kuwa na mahusiano bora baina ya mzazi na mtoto. Vitu
vichache cha kuzingatia
1. Waonyeshe na kuwahakikishia upendo wa
kweli. Wasaidie kupunguza au kuondoa hofu wanapokuwa na wewe au kuongea
na wewe, watoto wako wanatakiwa wakuheshimu kwa upendo sio kukuogopa.
Endelea..........http://chrismauki.blogspot.com/p/education.html
No comments:
Post a Comment