Tafiti
zinaonyesha kwamba kemikali zinazo achiliwa mara baada ya mwanamke kufikia
kileleni “ejaculation” wakati wa tendo la ndoa (oxytocin and dopamine) humfanya
mwanamke kutamani kuendelea kuwa macho, kuongea na mpenzi wake au kuendelea
kupapaswa na kukumbatiwa. Bahati mbaya kwa upande wa pili mshindo huu au
kuachiliwa kwa kemikali hizi huwa kama vile kidonge cha usingizi kwa mwanaume na
hivyo kumfanya kupotelea usingizini hata bila kutoa taarifa. Jambo hili limewakwaza
wanawake wengi wakitafsiri kuwa wanaume hawawajali na hawako tayari kuwa na
hata maongezi kidogo mara baada ya wao kujitosheleza kuhisia. Sasa ni vema
wanawake kujua katika hili kwamba ukiona kapotelea usingizini hajapenda,
kazidiwa, ingawa na sisi wanaume tufahamu kuwa kuendelea kuwa naye macho mara
baada ya kumaliza shuhuli ni zawadi nzuri sana kwake. Jitahidi – Chris Mauki
No comments:
Post a Comment