Kunatofauti kubwa sana kati ya kufanya kazi na kufanya
kazi unayoipenda na uliyoitamani tokea mbali. Zaidi ya asilimia 85 ya watu
hufanya kazi wasizozipenda au ambazo hawakuwahi kuzitarajia kuja kuzifanya na hii
inawapa kukosa furaha na utoshelevu “satisfaction”
katika kile wakifanyacho hata kama kinaonekana ni kizuri na chenye kuwalipa.
Ogopa sana na epuka kabisa kuishia kwenye kazi au ajira ambayo huna mapenzi
nayo tokea moyoni mwako, usije kuishia kukifanya kile unachokipenda na
kukitamani ukishastaaafu hicho unachokifanya sasa, kwamaana muda wakukifanya
kile ukipendacho utakuwa ni mdogo na mfupi sana wakati ulifanya usichokipenda
kwa muda mrefu maishani mwako. Kati ya vitu viwili muhimu kuvifurahia maishani
ni familia yako, na kazi unayoifanya. Jifunze kufanya chaguzi bora, kuweka
malengo bora na kufanya maamuzi bora iwapo mapema – Chris Mauki.
No comments:
Post a Comment