CHRIS MAUKI
B.A Education, M.A A.S.P: UDSM. PhD
candidate in Social psychology & counseling: University of Pretoria. SA
§ Assistant lecturer in Social psychology and Counseling,
KWA KISWAHILI
CHRIS MAUKI
B.A Education, M.A A.S.P: UDSM. PhD candidate in Social psychology & counseling:
Chris Mauki ni mkufunzi msaidizi
katika idara ya saikolojia ya chuo kikuu cha Dar es Salaam. Chris ni mtaalam na
mwalimu wa saikolojia ya jamii pamoja ushauri wa kisaikolojia. Mbali na
kufundisha ushauri wa saikolojia Chris Mauki pia amewasaidia wengi kupitia
ushauri wa kisaikolojia (professional counseling) katika maeneo mbalimbali ya
maisha kama vile ndoa, mahusiano, matatizo ya kitabia, uzazi na malezi,
matayarisho ya kustaafu, ushauri wa mambo ya kazi, namna za kuishuhulikia
misongo ya mawazo, na mengine mengi. Kwa utaalamu wake wa saikolojia ya jamii
na ushauri wa kisaikolojia Chris Mauki amefanya kazi kwa karibu sana na taasisi
nyingi za kiserikali na zisizo za kiserikali. Kwa sasa Chris Mauki pia ni
mtaalam mshauri wa kampuni ya ICAS South Africa inayoshuhulika na masuala ya
kisaikolojia ya wafanyakazi wa taasisi za fedha hapa nchini.
Chris Mauki mekuwa akitumia muda
wake mwingi katika mikutano ya uhamasishaji wa masuala ya maisha (motivational
talks), badhi ya mikutano na makongamano haya yamekuwa yakiandaliwa nayeye
mwenyewe, na mengine mengi amekuwa akitumika kama mzungumzaji mwalikwa. Maeneo
ambayo amekuwa akiyazungumzia na kuyafundisha kwenye mikutano na makongamano
haya ni kama vile; Njia bora na malezi, mahusiano, usuluhishi na utatuzi wa
migogoro katika mahusiano, mbinu za kuukomboa na kuutumia muda kiufanisi, jinsi
ya kujiwekea mipango na malengo katika maisha, maisha baada ya maisha ya
chuoni, uongozi, saikolojia ya watoto, na mbinu za maendeleo binafsi. Baadhi ya
mafundisho haya yanapatikana katika mfumo wa santuri (CD na DVD). Kitabu chake
cha kwanza kinachozungumzia mambo haya kwa undani zaidi kiko katika
matayarisho.
Katika jitihada za kutanua wigo
wa vipawa na talanta zake Chris Mauki amejihusisha sana na vyombo vya habari.
Kwa zaidi ya miaka mine amekuwa akiendesha program inayoitwa “Saikolojia ya Maisha” katika kituo
cha Praise Power Radio 99.2 FM, mara kwa mara amekuwa mwalikwa katika
mazungumzo maalum katika vituo vya Clouds FM, WAPO FM, East Africa Radio na
vingine pia. Chris Mauki amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Televisheni
kiitwacho Five Connect (5connect) kinachorushwa na EATV ambacho kimekuwa
kikishuhulikia mambo mengi yahusuyo vijana na maisha ya kilasiku. Mbali na
redio na televisheni Chris Mauki pia amekuwa akiandika makala zihusuzo
saikolojia ya maisha katika magazeti ya Global Publishers. Maisha ya wasomaji
wengi wa makala hizi, ndani na nje ya Tanzania yamebadilika na kuboreka
zaidi.
Pamoja na majukumu mengine nje na
kazi za kitaaluma, Chris Mauki anahusika pia na kupanga na kuratibu shuhuli na
matukio mbalimbali (MC), yakiwemo ya kiserikali, makampuni na ya kijamii. Chris
Mauki amekuwa msaada pia katika kazi za kutafsiri lugha za kiingereza na
Kiswahili (oral and written).
Kielimu, Chris ana shahada (BA)
ya sanaa na elimu, shahada ya uzamili (Masters) ya saikolojia ya jamii na sasa
yuko masomoni katika shahada ya uzamivu (Ph.D) ya masuala ya matatizo ya ndoa
na madhara kwa watoto.
Kimajukumu, Chris Mauki anafuraha
kuwa mume wa Miriam Lukindo Mauki na wawili hawa wamebarikiwa watoto wawili wa kike Rommy na Ronel
No comments:
Post a Comment