Haijalishi
sana jinsi ndoa yenu ilivyokuwa siku mlipokuwa mnaoana, kinachojalisha zaidi ni
katika jinsi mnavyoishi wawili ndani ya ndoa hiyo, kiukweli inawezekana kabisa
ndoa yenu ilikuwa ni story ya mjini, ukumbi wa garama sana, mapambo bei
hielezeki, mc the best of the town, gari yenu peke yake ilikuwa bajeti ya
harusi ya mtu mwingine na hanymoon mkaenda ulaya, Dubai au Capetown au kokote
unakohisi ni kwa gharama na pa kuvutia sana, lakini ukiyaangalia maisha
mnayoishi wote baada ya matumizi haya yote ya fedha za wasamaria wema walioamua
kuzipotezea kwenu, unaona furaha ile iliishia ukumbini au ilidumu kwa
wikichache sana baada ya fungate, machungu na maumivu ya moyo unayoyapitia
yanakufanya uone aibu hata kuziangalia picha zenu na mikanda yenu ya harusi.
Sio bestman, matron wala wazazi wenu wanaojua chungu mnayoipitia, ukiuangalia
moyo na nafsi yako unatamani kuilaani siku ile uliyomkumbatia na kucheza naye
muziki wa taratibu ukumbini huku watu wakidhani “wapendanao wawili wamekutana”.
Ngoja nikutie moyo, najua kweli kuna sehemu ulikosea au mlikosea, najua majuto
karibu yafunike matarajio yako, lakini lipo tumaini, maadam bado mnapumua, basi
mnaweza kuyarekebisha na mkaiona tena ile furaha ya mwanzo kama kweli wote
mnadhamiria kuitafuta furaha hiyo. “It
takes two to tango” Pasipo nia ya dhati ya wote wawili, furaha hii bado
itakuwa ni kitendawili. Nyanyuka, futa machozi, chukua hatua, tumaini bado lipo
– Chris Mauki.
Follow CHRIS MAUKI:
Facebook