Follow CHRIS MAUKI:

www.chrismauki.com

Thank you very much for visiting our blog. We have new website for you,we are sure this new website will completely blow your mind! Subscribe by entering your e-mail below to stay updated on our progress.

Launching
comeback
launchpad

Tuesday 3 June 2014

CHIMBUKO LA WANAUME KUSEMA UONGO KWENYE MAHUSIANO



Imegundulika na kuhakikiwa kwamba uongo ni mbinu mojawapo muhimu sana inayotumiwa na wanaume wenye lengo la kutafuta fursa za kupata mpenzi au wapenzi ili kufanya mapenzi yasiyo ya kudumu na yasiyo na uwajibikaji “short term partners”. Kila wanaume watatu kati ya wane walioshiriki utafiti huu walikiri kuwa wakotayari kutumia uongo au kupindisha ukweli ili tu kuweza kupata fursa ya kufanya mapenzi. Mambo ambayo wanaume hudanganya yanafanana karibu katika kila jamii na tamaduni, kwa mfano; wanaume wengi huongeza chumvi au kukuza taarifa wanapoongea habari ya vitu wanavyomiliki, wanapoongea kuhusu nafasi zao kazini au kwenye jamii (kama yeye ni mfanyakazi wa kawaida atamwambia mpenzi wake kuwa yeye ni meneja au ndio mwenye kampuni), wengine hudanganya kuhusu biashara zao (yamkini wala sio zao, ila wanajishikiza tu) au wanasema uongo kuhusu kujulikana kwao (yeye kila mtu maarufu anamjua au ni rafiki yake). Kwa kuangalia hili inaweza kukupa tahadhari wewe msichana au mwanamke kwamba ukiona uongo unashika hatamu katika hatua za mwanzoni fahamu kabisa kuwa wewe unaandaliwa kuwa “temporary or part time partner”. Tatizo wengine mko tayari kudanganywa kwasababu mkiambiwa ukweli eti mtaumia, we haya we!!!! – Chris Mauki

No comments:

Post a Comment

KWA USHAURI ZAIDI

Email : chrismauki57@gmail.com
Mob No:+255713 407182

Total Pageviews

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
+255718-243339 or +255713-407182 / chrissmauki2014@gmail.com
Powered by Blogger.

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

JITAMBUE KISAIKOLOJIA

Popular Posts

About Me

Blog Archive